‘Addicted hit maker’ Hussein Machozi amefunguka kuhusu
uhusiano wake na Diamond platnumz na kuonesha kuwa hawana urafiki hata kidogo,
japo hakusema moja kwa moja kama wana uadui na kwamba yeye na Diamond ni kama
‘Jogoo na kuku Jike’ na yeye Hussein ndiye jogoo!
Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi amefunguka kwenye XXL
ya Clouds fm katika segment ya U Heard, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu
tuhuma zilizowafikia ‘Timu Makorokocho’ kuwa Hussein Machozi alipigana na
Diamond Platinumz huko Mombasa.
Japo Hussein alikiri kuwa anauwezo wa kupigana kama bondia,
lakini alikanusha kabisa kuwa hajawahi kupigana na Diamond na wala hajawahi
kuzinguana nae, kwa sababu hawajawahi kabisa kuwa karibu, na sababu ni kwamba
wanatokea katika sayari tofauti kabisa, yeye anatokea sayari nyingine na hajui
Diamond anatokea sayari gani.
Japo aliongea kwa ufupi sana lakini hii ilitoa picha ya moja
kwa moja kuwa inawezekana Hussein ana kitu moyoni ama hasira flani kuhusu
Diamond Platinumz. Je wewe unamtazamo gani kuhusu hili?
tagazo
No comments:
Post a Comment