Baba mtakatifu Benedikti wa 16
Katika
hali isiyotegemewa, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki lenye kusadikiwa
kuwa na wastani wa waumini billioni 1.2 duniani kote ; kiongozi huyo,
baba mtakatifu Benedikti wa 16 ametangaza kujiuzulu. Sababu zilizotolewa
kutoka kwa msemaji mkuu wa Vatican Padre Frederico Lombard, washirika
la wamisionari Wajesuit ameuthibitishia ulimwengu kuhusu habari hizo
kupitia radio Vatican. Sababu za Kiumri na kiafya ni baadhi ya sababu
zilizohusishwa na kujiuzulu huko.
Baba
mtakatifu Benedikti wa 16 alizaliwa 1927 na kubatizwa jina la Joseph
Ratzinger. Amekuwa Pope wa 265 katika mlolongo wa viongozi wa kanisa
hilo.
Ratzinger alikuwa na umri wa miaka 78 wakati alipochaaguliwa kuliongoza kanisa hilo mwezi April 2005.
Hakuna
Pope ambaye amejiuzulu kwa hiari katika nyakati za hivi karibuni na Pope
wakwanza kuachia ngazi alikuwa Pope Gregory XII mnamo mwaka 1415;
yapata miaka – 598 iliyopita. Kabla ya yake Pope mwingine aliyejiuzulu
kwa hiari ni Pope Celestine V mnamo mwaka 1294.
Kiongozi
huyo mwenye asili ya Ujerumani, ametangaza uamuzi huo akiwa na umri wa
miaka 85. Baada yakuliongoza kanisa Katoliki kwa takribani miaka nane
ametangaza kuachia ngazi ifikapo tarehe 28/02/2013. Na habari kutoka
vyanzo mbali mbali zinasema kuwa huenda kiongozi mpya wa kanisa hilo
akachaguliwa ifikapo mwishoni mwa mwezi March mwaka huu.
Anakuwa
kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo Katoliki kujiuzulu baada ya takribani
miaka 600, iliyopita wakati kiogozi wakanisa hilo alipojiuzulu.
Alichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa hilo mwezi April 19, 2005 wakati
huo alikuwa na umri wa miaka 78 – akimzidi mtangulizi wake wa kiti hicho
baba mtakatifu Yohane Paulo II kwa miaka 20 wakati alipochaguliwa
kiongozi wa kanisa hilo.
Alikuwa
pope wakwanza kutoka Ujerumani kwa takribani miaka 1,000 iliyopita, na
ni pope wapili asiye muitaliano katika mlolongo wa viongozi wakanisa
hilo. Aliweza kusafiri nje ya Itali walao kwa wastani mara nne kwa mwaka
lakini hakufikia rekodi ya mtangulizi wake.
Pamoja na
changamoto nyingi alizokutana nazo wakati wa uongozi wake ikiwemo zile
za ubakaji wawatoto. Kiongozi huyo aliweza kusimamia vizuri kile
kinachoitwa “family values” na alipinga kwa nguvu zote utoaji mimba,
ndoa za jinsia moja na « euthanasia » yaani kuwaondolea uhai wale
wanaosadikiwa kuwa na maumivu makali au umri ulichoka sana. Uhai wa
binadamu ikiwa ni moja ya thamani aliyopewa binadamu toka kwa muumba
wake yaani mwenyezi Mungu. Kiongozi wakanisa hilo huchaguliwa na
viongozi wa juu wakanisa hilo maarufu kama ma-kardinali. Ambaye kwa
Tanzania itawakilishwa na Kardinali Pengo.
Afrika
inakardinali ambaye anaweza kufikiriwa na wachaguzi hao. Ambaye ni
Kardinali Peter Turkson(64) ambaye pia ni mkuu ya depatimenti/idara ya
Haki na Amani katika Vatican. Huzungumza kwa ufasa lugha za Kifante,
Kiingereza, Kifaransa, Kiitaliano, Kijerumani, Kiebrania, Kiaramaiki,
Kiarabu na kigiriki.
Nimezaliwa wa Ghana. Aliteuliwa kuwa Kardinali mwaka 2003.
Kardinali
mwingine anayeweza kufikiriwa kutoka Afrika, japokuwa umri unamtupa
mkono ni Kardinali Francis Arinze, 80, kutoka Nigeria pia ni chaguo
wezekano kuongoza kiti hicho.
Mzaliwa
wa Nigeria, 1932, the 80- anaweza kuwa mwafrika wa kwanza katika kipindi
cha miaka 1,500 kukalia kiti hicho cha mtakatifu Petro. Kardinali
Arinze alipewa daraja la Upadri 1958 na akawa askofu wakwanza kijana
duniani kote akiwa na miaka 32, mwaka 1965. Aliteuliwa kuwa Kardinali
mwaka 1985.
Wakati
huo huo viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa siasa na dini mbali
mbali wameupongeza uamuzi huo wabusara na kumtakia afya njema kiongozi
huyo. Viongozi hao ni pamoja na waziri mkuu wa Uingereza ndugu David
Cameron, Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel, chifu rabbi Yona
Metzger wa Israeli, rais wa Ufaransa ndugu François Hollande na wengineo
wengi.
Ifuatayo
ni sehemu ya ujumbe wa baba mtakatifu uliotolewa kwalugha ya kilatini
kwa viongozi wa “consistory”, au baraza la viongozi wa kanisa hilo,
akitangza mpango wake huo wakujiuzulu leo jumatatu asubuhi. Ujumbe huo
unasema:
"Dear Brothers,
I have
convoked you to this Consistory, not only for the three canonizations,
but also to communicate to you a decision of great importance for the
life of the Church. After having repeatedly examined my conscience
before God, I have come to the certainty that my strengths, due to an
advanced age, are no longer suited to an adequate exercise of the
Petrine ministry. I am well aware that this ministry, due to its
essential spiritual nature, must be carried out not only with words and
deeds, but no less with prayer and suffering.
However,
in today's world, subject to so many rapid changes and shaken by
questions of deep relevance for the life of faith, in order to govern
the bark of Saint Peter and proclaim the Gospel, both strength of mind
and body are necessary, strength which in the last few months, has
deteriorated in me to the extent that I have had to recognize my
incapacity to adequately fulfil the ministry entrusted to me.
For this
reason, and well aware of the seriousness of this act, with full freedom
I declare that I renounce the ministry of Bishop of Rome, Successor of
Saint Peter, entrusted to me by the Cardinals on 19 April 2005, in such a
way, that as from 28 February 2013, at 20:00 hours, the See of Rome,
the See of Saint Peter, will be vacant and a Conclave to elect the new
Supreme Pontiff will have to be convoked by those whose competence it
is.
"Dear
Brothers, I thank you most sincerely for all the love and work with
which you have supported me in my ministry and I ask pardon for all my
defects. And now, let us entrust the Holy Church to the care of Our
Supreme Pastor, Our Lord Jesus Christ, and implore his holy Mother Mary,
so that she may assist the Cardinal Fathers with her maternal
solicitude, in electing a new Supreme Pontiff. With regard to myself, I
wish to also devotedly serve the Holy Church of God in the future
through a life dedicated to prayer."
Imeandaliwa na Frederick Meela, kwa msaada wa vyanzo mbalimbali.
Ndugu yenu kabisa wa Francophonie, tawi la Ufaransa.
No comments:
Post a Comment