Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa matumizi
mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la
uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya
ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’,
‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana
na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga
mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine
ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona
kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na
‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha
wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya
biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa
ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa
‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko
Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha
biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter,
BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza
mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika,
zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza
ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya
kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya
biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti la Mwananchi
walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na
kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba
zao kwenye mtandao.
No comments:
Post a Comment