Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe
Dar es Salaam.
Kauli ya Tanzania inakuja huku kukiripotiwa kuwapo kwa mapigano
makali baina ya vikosi vya Serikali waliopambana na waasi hao, ambao
wameanzisha tena harakati ya kuliteka Jimbo la Goma na maeneo mengine ya
jirani.
Mapigano hayo ni ya kwanza tangu M23, kuondoka mjini humo mwaka jana kufuatia shinikizo za kidiplomasia.
Umoja wa Mataifa (UN), umesema utaongeza kasi ya juhudi zake za
kutafuta amani kwa kutuma kikosi cha wanajeshi 3,000 kujaribu kuzima
mapigano hayo, ambayo yalisababisha watu 19 kuuawa na wengine
kujeruhiwa.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala
Mgawe alisema vikosi vya Tanzania vilivyoko Congo vitaendelea kutekeleza
majukumu yake kwa kuzingatia weledi na miongozo ya UN.
Kanali Mgawe alisema kauli zozote za vitisho vinazoendelea kutolewa na waasi hao, haziwezi kurudisha nyuma juhudi hizo.
Hata hivyo, Kanali Mgawe aliitaka Jumuiya ya Kimataifa kutopuuzia vitisho hivyo.
“Inawezekana kuna jambo hapa maana kwa nini Tanzania ipewe
vitisho ilhali operesheni hiyo ya amani inahusisha mataifa mengine?”
alihoji Kanali Mgawe.
Nchi nyingine ambazo zimekubali kutuma wanajeshi wake kupigana na waasi hao ni Malawi na Afrika Kusini.
Waasi wa M23 wamekuwa wakitoa vitisho kwa wanajeshi wa Tanzania,
lakini Serikali imekuwa ikitamba kuwa hivyo ni vitisho na kazi ya
kulinda amani itaendelea kama ilivyopangwa. Tayari, Katibu Mkuu wa UN,
Ban-Ki Moon ametembelea nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment