Thursday, June 27

ULINZI WA OBAMA HAUJAWAHI TOKEA AFRICA



Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.

No comments:

Post a Comment

Search This Blog