Wednesday, July 24

MJANE ALIYETIMULIWA KATIKA MSIBA WA MWANAJESHI WA JWTZ AJITOSA TENA KUHUDHURIA MAZISHI YA MUMEWE


FAMILIA ya Marehemu, Fortunatus Msofe, ambaye ni mmoja wa wapiganaji wa JWTZ, waliofia Darfur, wamemzuia aliyekuwa mchumba wake Amina Juma kushiriki katika mazishi na kumfungia mlango wa nyumba ya marehemu asiingie ndani mara tu baada ya taarifa za kifo cha marehemu kuwafikia.  

Hata hivyo Amina amelazimika kwenda Tanga kushiriki shuguli za mazishi ya marehemu pamoja na kwamba familia ya marehemu haitaki kumuona katika msiba huo.

Akizungumza na gazeti moja la kilasiku la kiswahili nchini Tanzania, Amina alisema kwamba ingawa awali alikata tamaa ya kumzika mwenzake, lakini jana aliamua kwenda Tanga kuhudhuria mazishi na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya kujishauri sana.


Baba wa marehemu, Wilbad Msofe aliiambia gazeti hilo kutoka Kange, Tanga kuwa alishangazwa na hatua ya Amina kutowafahamisha  kuhusu msiba huo. Alisema hiyo ndiyo sababu za yeye kuamua kutaka mwanawe apelekwe Kange kwa mazishi.

Akizungumza na gazeti hilo akiwa njiani kwenda Kange, Amina alisema: “Nilikuwa ninataka sana kumzika mwenzangu lakini ile hali  ilikuwa imenichanganya pamoja na kwamba nilishauriwa, sasa nimekata shauri nakwenda Tanga.
  
“Najua kuna kitu hapa, lakini ‘Fortu’ kwa kuwa nilikuwa naye, na wana ndugu wa upande wa wake wameshanikana, mimi nitamzika tu  mwenzangu na kurudi,” alisisitiza.  

Miili ya wapiganaji hao iliagwa jana katika Makao Makuu ya Jeshi, yaliyoko Upanga na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi  Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, makamanda na wanajeshi walishiriki kuwaaga wanajeshi hao.

Akizungumza kwa masikitiko na huku sauti ikiwa imemkauka kutokana na kulia muda mrefu, Amina alisema: “Siwazii mtafaruku uliopo,  moyo umenituma kwenda kumzika mume wangu, niliwaza usiku kucha na leo (jana) Jumatatu asubuhi nikaamua kwenda Tanga.”


“Msofe amekufa tulikuwa tuna mipango mingi, tulipanga harusi kubwa lakini haikuwahi kufanyika, niliongea naye alfajiri ya Jumamosi  ya Julai 13, akaniambia tutaongea baadaye maana wanakwenda kwenye operesheni...


“Unajua tuliishi maisha ya kipekee sana tulipendana kiukweli hata majirani tuliokuwa tukiishi nao Mbezi na Visiga wanajua hilo na wengi walikuwa wakinisihi sana nisije kumuudhi huyu kijana. 

"Nafsi  inauma sana. Nawashangaa  wazazi  wake  kwa kunikana" 

No comments:

Post a Comment

Search This Blog