Thursday, July 16

JE, UNATAKA KUISHI KWA FURAHA NA MPENZI WAKO?

je, Unataka kuishi kwa furaha na mpenzi wako ?

Katika mahusiano ya wanandoa, wapenzi au wanaoishi pamoja yanaweza kudumishwa kutokana na upendo uliojengwa kwa misingi ambayo inabidi ifwatishwe ili kufikia lengo. Mahusiano huwa yanatofautiana kwa jinsi kila mtu anavyoyachukulia kwa maana hiyo hamna sheria kuu ya kuyaongoza bali huwa kuna muongozo ambao japo unakuonesha njia sahihi ya kuweza  kuwafanya mfike mbali na muwe na  furaha.
Muongozo huu umejengwa ama umetokana na mikasa ya maisha ya kila siku iliyotokea  kwa  wenye mahusiano ili isipate kujirudia hali ya kutokuwa na maelewano wala furaha. Muongozo huo ama sababu hizo ni kama;

Kuachana isiwe suluisho la kwanza
Ukiuliza sehemu mbali mbali kuhusu njia gani ya kusuluhisha matatizo kwa wapenzi ama wanandoa utasikia “acha nae tafuta mwengine”, hili ni kosa kubwa sana kwa kuwa utakuta mtu anaingia kwenye mahusiano au ndoa huku akilini kashaweka  kuwa ukizingua muda wowote naweza kukuacha. Mahusiano haya hayawezi kudumu muda mrefu kwa kuwa kila mmoja takuwa anatafutia sababu mwenza wake pindi pale wanapokorofishana ili aweze kujitoa badala ya kujaribu kulitatua tatizo. Inabidi   uwe makini na upige moyo konde ukidhamiria kusuluhisha ili nyote muwe na furaha ya kweli.
Relationship-wapenzi-wanagombana-kitandani

Mahusiano yaendane na kila aina ya hali
Hamna mtu anayeweza kusema kuwa mahusiano yake yamekamilika kwa kuwa  mapungufu hayakosekani. Unaweza ukasema furaha ipo katika mahusiano yenu kwa kuwa labda kipato chenu ni kizuri kwa wakati huo ila hali ikibadilika inaweza ikawa chachu ama sumu ya kuharibu mahusiano yenu kwa kuwa labda mmoja wenu hajazoe kuishi katika hali duni. Katika maisha kuna kupanda na kushuka, hivyo basi hamna budi kuvumiliana kwa shida na raha. Watu walio kwenye mahusiano wakiweza kubalance nyakati za shida na raha hao ndio wanaweza kuwa na mahusiano yenye furaha siku zote na uhusiano wao ukadumu zaidi.
Relationships-mpenzi-omba-ruhusa-kuongea

Usijenge hofu kwa mwenzako ama kwake pia
Sababu nyingine ya kuwa kwenye mahusiano yenye furaha ni kuwa muwazi kwa mwenza wako . Kuwa huru kujielezea kwa mwenzako na wakati huo huo mfanye mwenzako asiwe na uwoga wa kukueleza jambo lolote kiuwazi akihofia malumbano.  Mara nyingine mkielezana jambo linalowatatiza kwa muda huo linaweza kuisha kiurahisi kuliko hata mlivyotegemea ila ukiweka duku duku  na ukikaa kimya bila kuzungumza na mwenza jambo linaweza likakuwa kubwa siku nyingine ikawa shida kusuluhisha.Hii inaondoa dhana ya nidhamu ya uwoga, hata mwenzako akikosea inakuwa rahisi kumwambia ili ajirekebishe na mambo yaweze kuendelea bila matatizo yoyote.
relationship-nataka-space

Kumuheshimu,kumjali na kumpenda kwa vitendo mwenza wako
Mara nyingi siku hizi imekuwa rahisi sana kumwambia mwenza wako neno “nakupenda” ila upendo wako unakuwa hauambatani na vitendo vinavyoendana na hali hiyo. Neno “upendo” hua haliji peke yake bali huwa linakuja na furushi la mambo yanayofanya neno lenyewe likamilike. Mambo yenyewe ni kama heshima, kujali, kushirikishana, kujitoa kwake kwa hali mali na kusameheana pindi mmoja anapoteleza au kukosea. Onyesha hisia zako za kweli kwa mwenza wako ili aweze tambua uzito wa upendo wako kwake. Ukizingatia hayo basi bila shaka utakua na furaha kwenye mahusiano.
Relationships-kamilifu

Muwe kitu kimoja siku zote
Hata siku moja usije jaribu kutokuwa upande wa mwenza wako ama kutomuunga mkono kwenye mambo mbali mbali. Kwenye jambo jema muunge mkono na uzidi kumpa moyo na kwenye jambo ambalo unaona litakuwa baya kwake usimwache hivi hivi bali mshauri ili aweze fikia shauri jema. Kama mkiwa wenyewe kwenye mazingira ya peke yenu mnalumbana kuhusu mjadala flani  mpaka ikafikia hatua ya kukubaliana ama kutokubaliana basi iwe  ni kati yenu lakini mkiwa mpo kwenye umati wa watu wote muwe na sauti moja kuhusu mjadala huo. Hii huwa inasaidia sana kuimarisha mahusiano yenu  ukizingatia kama mmoja wenu mjadala huo mlimvunja moyo na kumfanya asiwe na raha mbele za watu. Kuwa na msimamo mmoja pia itaonyesha jinsi gani nyinyi nyote jinsi gani upendo wenu ulivyoshiba na pia furaha lazima itapata chimbuko la kutokea.
Relationships date


No comments:

Post a Comment

Search This Blog