Katika maisha ya kawaida imezoeleka kuona watu wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na hatimaye wengine kufikia hadi kufunga ndoa ila kunawengine hawatekelezi hata kimoja kati ya hivyo. Hii inaweza kuchangiwa na sababu mbali mbali ambazo zinaweza kuwa kikwazo ama wengine kupendelea hivyo. Takwimu zinaonyesha kuwa kadiri ya siku zinavyokwenda ndivyo idadi hii inaongezeka kutokana na mabadiliko yanayoweza kuwa ya kiuchumi ama ya kijamii kiujumla. Baadhi ya sababu hizo zinaweza kua;
Ugumu wa maisha
Kutokana na jinsi ilivyozoeleka katika jamii kuwa mwanaume ndio mtafutaji, sasa na jinsi hali ya maisha inavyozidi kupanda ndipo inapompelekea na yeye kufanya kazi zaidi ili aweze kwenda nayo sawa huku akijikimu na mahitaji yake. Hali hii inaweza kumfanya awe anafanya kazi muda wote kupelekea mpaka kukosa mda wa mahusiano au hata akiwa kwenye mahusiano inakuwa kuonekana ni vigumu sana kutokana na mihangaiko. Hii inaweza kuchangia pia mtu kutotaka kuwa kwenye mahusiano.
Uhuru wa mtu binafsi
Kila binadamu huwa anapendezwa na uhuru wake yeye binafsi na kuweza kufanya mambo yake bila kushurutishwa na mtu. Sasa kutokana na uhuru huo, kuna wengine wanauchukulia kivingine na kuwa wabinafsi kwa kumaanisha kwamba anakua hayupo tayari kujitoa na mwenzake,kumjali au kutaka kujenga maisha na mwenzake akiamini kuwa itamrudisha nyuma kimaendeleo, bado anataka kuendelea kujenga maisha yake. Hii inaweza ikawa kichocheo pia cha kufanya watu kutotaka kuwa kwenye mahusiano.
Kujiongeza kielimu
Ni vizuri sana kupenda kuongeza elimu ili kuwa na ufahamu mkubwa katika mambo mbali mbali na hata kusaidia jamii yako kutokana na elimu uliyoipata. Ila wakati mwengine elimu isizidi maarifa kwa kuwa Utakuta watu wengine wanakua na hamu ya kuendelea na elimu huku wakisahau kabisa kuhusu maisha ya kijamii yani kuwa na mahusiano,kujichanganya na watu au kutaka kuanzisha familia. Kama unavyojua elimu huwa haina mwisho kwa kuwa vitu vipya vinatoka kadiri kila mara ambavyo vinahitaji uelewa wetu. Usipoangalia unaeza ukajikuta umri umekwenda na bado upo peke yako bila na matumaini ya kuwa na mwenza wala ya kuanza familia.
Kuvunjika kwa mahusiano
Hii naweza kusema kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha watu kutaka kubaki peke yao bila kuwa na mahusiano kama ya ndoa ama ya kawaida kutokana na maumivu waliyoyapata na uhusiano waliotoka. Watu wengi huwa wanaishi kwa kusonga mbele huku wakizingatia kule walipotokea ili kuhakikisha yasijirudie makosa. Utakuta mtu hataki tena kuwa kwenye ahusiano kwa kuwa anakumbuka shida,tabu, manyanyaso ama kutokua huru. Kwa kuwa ameshaonja chachu hiyo, wengi huwa wanakua hawapo tayari kurudi tena katika hali hiyo, anaona bora abaki mwenyewe.
Kutokua na uwezo wa kujitoa kwa mwenzako
Kuna watu wengine wanakuwa hawapo tayari kujitoa kwa hisia kwa mwenza wake yani anakua mgumu kwa kila kitu hasa tukiangalia kwa upande wa fedha. Wanaume wengi wamekuwa wakiogopa kujiingiza katika ndoa kwa kuwa wanafikiria siku atakapo achana nae atalazimika kugawana nae mali. Hii huwa ni fikra mbaya ambayo pia huchochea kwa namna kubwa sana wao kubaki peke yao na kutojihusisha kwenye mahusiano.
No comments:
Post a Comment