Mojawapo ya maswali ambayo nimekuwa nikiyapata kutoka kwa baadhi ya wanaume ni kutaka kujua kama ni saizi gani ya maumbile yanayoweza kumridhisha mwanamke. Wengi walidai kwamba wanahisi kwamba maumbile yao ni madogo na wana mashaka kama wanawatosheleza wapenzi wao au wake zao.

Kwa upande wa wanawake wao wameonekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kama maumbile makubwa ndiyo yanayoridhisha ukilinganisha na maumbile madogo? Huu ni mkengeuko mkubwa wa tendo la kujamiiana kutokana na jinsi watu wanavyolichukulia tendo hilo. Hata hivyo nililazimika kuwadadisi baadhi ya walionipigia simu kutaka kujua chanzo hasa cha hofu hiyo. Je wenzi wao waliwahi kuwalalamikia kuhusu kutoridhishwa kwao na tendo la kujamiiana?

Ukweli ni kwamba wengi walikiri kuwa wenzi wao hawakuwahi kuwalalamikia, lakini kutokana na simulizi wanazozisikia kutoka kwa watu mbalimbali, kuna madai kwamba wanawake wanapenda maumbile makubwa, Pia walikiri kuangalia mikanda ya video ya ngono na kuona jinsi wanaume walivyo na maumbile makubwa kushinda ya kwao na ndio chanzo cha wao kupata hofu kwamba huenda wenzi wao hawaridhishwi na maumbile yao. Niliendelea kudadisi, Je wanataka ukubwa wa saizi gani kwa vipimo halisi. Kwa bahati mbaya hakuna aliyeweza kujibu swali hilo, wengi walikuwa wanababaika tu na hakuna hata mmoja aliyekuwa na majibu sahihi.

Kwa upande wa wanawake wao nao walikiri kwamba simulizi wanazopeana kuhusu tendo la kujamiiana pale wakutanapo kwenye vikao vyao, (pengine kwenye saluni), nako mambo ni hayo hayo, hujadili kuhusu saizi ya maumbile inayoweza kumridhisha mwanamke. Kwa bahati mbaya kuna kudanganyana kwingi kuhusu ukubwa wa maumbile ya wanaume na ridhiko la tendo la kujamiiana na ndio sababu wale vijana wa wanaosifiwa huko mitaani kuwa wana maumbile makubwa wamekuwa wakiwapata wanawake kirahisi kutokana na kila mmoja kutaka kujua kama atapata ridhiko tofauti na alivyozoea…..! lakini swali bado linabaki pale pale. Je ukubwa wa uume unaozungumziwa ni upi?

Hebu tuone wataalamu wanasemje kuhusu kuhusu jambo hilo:

-Kwa wastani maumbile ya mwanaume yanatakiwa yawe na ukubwa wa kati ya inchi tano mpaka sita kwa urefu pale unaposimama.

-Pale ambapo hauyajasimama mwaumbile ya mwanaume yanatakiwa yawe na ukubwa wa inchi tatu mpaka nne kwa urefu

-Hata hivyo utafiti umebaini kwamba hakuna uhusiano kati a urefu wa mtu na maumbile ya uume wake………!

Utafiti uliofanywa kwa wanaume zaidi ya mia tatu, watafiti hao walibaini kwamba uume mkubwa ambao haujasimama ulikuwa na urefu wa inchi 5.5 na mtu aliyekuwa na uume huo alikuwa na urefu wa futi 5.7, uume mdogo kabisa uliopimwa ukiwa haujasimama ulikuwa na inchi 2.25, na mtu aliyekuwa na uume huo alikuwa na urefu wa futi 5.1.

Je urefu wa uume ndio unaoweza kumridhisha mwanamke katika tendo la kujamiiana?

Iwapo maumbile ya mwanamke yanamlazimu kupata uume mkubwa ili aweze kuridhika na tendo la kujamiiana, ni sawa, kwani kama wanaume wanavyotofautiana katika maumbile ya uume hata wanawake nao hutofautiana maumbile pia. Lakini wanawake wengi wamekiri kuridhishwa na maumbile yenye urefu wa kati ya inchi tano mpaka sita.

Watu wanapozungumzia ukubwa wa maumbile ya wanaume wanakuwa wamelenga urefu wa uume, lakini utafiti uliofanywa umebaini kwamba unene wa maumbile ya mwanaume ndio muhimu zaidi katika kumridhisha mwanamke katika tendo la kujamiiana.

Mwanasaikolojia Russel Eisenman akishirikiana na watafiti wenzie kutoka katika chuo cha Texas, Edinburg, waliwauliza wanawake 50 waliokuwa wakisifika kwa kushiriki sana tendo la kujamiiana. Wanawake hao waliulizwa, kama wao huwa wanaridhishwa na uume mrefu au mnene. Watafiti hao walishangazwa na matokeo ya utafiti wao. Kwani wanawake 45 kati ya hao 50 walidai kwamba huwa wanaridhishwa kimapenzi pale wanapokutana na mwanaume mwenya uume mnene. Ni wanawake watano tu kati ya hao 50 waliodai kuridhishwa na mwanaume mwenye uume mrefu.

Je ni kwa nini iwe ni maumbile manene ndiyo anayoonekana kuwaridhisha wanawake wengi………………?