Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi
karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume
anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa
ya Corner iliyopo Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo
cha vurumai hilo ni mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali
mwanamke huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na
mapema huku akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na
bwana wake huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana alikuja kishari na hata
alivyokuwa akiongea na yule bwana wake tulibashiri kutokea kwa ugomvi.
“Kweli… haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke
akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai
chanzo hicho.
Ikaelezwa kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema
waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia
kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo
hilo.
No comments:
Post a Comment