JIJINI Johannesburg na Mji Mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, jana (Julai 18), watu wengi walikusanyika sehemu mbalimbali kusherehekea siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya rais mstaafu wa nchi hiyo, Nelson Rolihlahla Mandela aliyetimiza umri wa miaka 95, huku hali yake kiafya bado ikiwa tete.

Pamoja na sherehe hiyo kutawaliwa na simanzi hadi kijijini kwake, Qunu katika Jimbo la Eastern Cape kufuatia afya ya Mandela au Mzee Madiba, makundi ya Waafrika Kusini yalikuwa yakimuombea apone.
Habari zilieleza kuwa sherehe hizo zilikuwa kubwa kwa kuwa Mzee Madiba aliandika historia ya mtu mweusi kuishi muda mrefu zaidi katika karne ambayo watu wenye umri mdogo wamekuwa wakifariki dunia kila kukicha.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, watu walikuwa wakiisubiri siku hiyo kwa shauku kubwa kwani wengi waliamini Mungu angejitwalia kiumbe wake kabla ya kutimiza umri huo.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kunong’ona kuwa serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikisubiri atimize umri huo ndipo waamuru madaktari waondoe mashine ndipo itangaze kifo chake.

No comments:
Post a Comment