Niko hapa bandari ya Mtwara kushuhudia mapokezi ya shehena ya kwanza ya mabomba ya gesi kutoka Uchina ambapo mgeni rasmi ni Mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu wa JMT, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Fuatana nami kujua kinachoendelea kupitia jf pekee, wengine watajua kuanzia usiku kwenye taarifa za habari za radio na TV, na kwenye magazeti ya kesho.

Karibu

Pasco.

===========
UPDATES:

Quote By Pasco View Post
Hivi sasa wageni mbalimbali wameishangia hapa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Col. Simbakalia (mjeshi/mjeda).

Wengine ni M/Kiti wa Bodi ya TPDC Bw. Michael Mwanda na bodi yake nzima, Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Bw. Yona Kilagane na menejiment team yake yote, Balozi wa China nchini na ujumbe mzito wa Wachina, wadau mbalimbali wa gesi asili, watu ambao naona kama wanamiss hapa ni wananchi wa kawaida!.

Kiukweli kama itatokea wananchi wa kawaida hawajaalikwa, Mkoa, Wizara na TPDC watakuwa wamerudia kosa lile lile la ushirikishwaji duni wa wananchi wa kawaida katika mipango mbalimbali ya maendeleo inayowahusu!.


NB: Pasco wa JF ni Mwanahabari wa kujitegemea kwa kujitolea, aliyejikita katika habari za kimaendeleo zenye maslahi kwa taifa kwa kuzingatia responsible journalism based on nothing but the truth, with objectivity na impartiality, na anaandika just for the love of it, not for making a living, hivyo halipwi na media yoyote ila sanasana yeye ni mwezeshaji kwa waandishi wachanga.