Monday, July 22

Majibu 16 ambayo hutakiwi kuyatoa kwenye interview unapokuwa unatafuta kazi! Part I

Worried businessman
1.  Swali: Ilikuwaje ukaacha kazi yako ya zamani?
Jibu: Mabosi walikuwa wazinguaji sana na nyodo zao ni za hali ya juu kumbe vidudumtu tu. 
2.  Swali: Tuambie tatizo lolote ambalo ulishawahi kupata mahali ukiwa unafanya kazi kutokana na mfanyakazi mwenzako na jinsi uluvyopenda litatuliwe.
Jibu: Kuna jamaa aliwahi kunisingizia nimeiba kazini. Niliomba wote tufukuzwe kazi. Mimi na yeye.
3. What are your hobbies and interests?
Jibu: Well, you know! Am  young and handsome and when I get the job I will have money and I love chics. So you know.
4. Why should we hire you? Kwa nini tukuajiri wewe na si mwingine?
Jibu: Well, unajua since the time I was at the university, mimi ni mtu wa party sana. Kwa hiyo kwa timu yenu ya events mimi nitakuwa asset nzuri sana. (WTF?!!!!)
5. Swali: Una swali lolote kwetu au kwa yeyote kati yetu?
Jibu: Yes. Kama wewe hapo ungekuwa wimbo wa Bongo Fleva, ungekuwa wimbo gani?
au Mngependekeza nifanye nini kama mvua inanyesha, usafiri shida na muda wa kufika kazini umefika bado sijafika? (Kazi huna ujue)
6. Swali: Kwa nini unahitaji hii kazi?
Jibu: Ninyi hamuoni maisha yalivyopanda bei jamani? au Baba kaniambia ni kazi nzuri. 
7. Swali: Kwa nini unataka kufanya kazi kwenye kampuni yetu?
Jibu: Mimi nataka hela tu jamani, wala nisiwadanganye., au Nimeona tu tangazo lenu Facebook nikasema ngoja nijaribu bahati yangu.
8. Unataka kuanza lini kazi?
Jibu: Ngoja kwanza niwasiliane na ndugu zangu halafu ntawaambia. 

No comments:

Post a Comment

Search This Blog