The Currently Biggest Bongo Flava Icon kutoka Tandale; Diamond platnumz a.k.a The president kutoka Wasafi classic, inasemekana ndiye msanii wa Bongo Flava anayefanya vizuri zaidi kimuziki kuliko wasanii wote nchini kwa sasa!
Hit-songs anazo-make kila kukicha;
Kama
vile Mbagala, nitarejea,Moyo wangu, mawazo, nimpende nani, lala salama,
na nyingine nyingi ndizo zimemwezesha msanii huyu mwenye Umri mdogo
kuweza kupata mialiko mingi ya kufanya shows nyingi nchini na ughaibuni;
mfano Napoly-Italy, London, Na Washington DC alikoenda hivi karibuni.
ani za msanii Diamond Platnumz) (moja ya video za zam
Historia ya muziki wake ni ya kuhuzunisha na kutia majonzi kama alivyoielezea katika wimbo wake wa Binaadam Wabaya ..ambao ulifanya vizuri katika anga la muziki hapa nchini na nchi za jirani..
Hata
Hivyo jitihada zake zimemsaidia kumfikisha katika malengo yake ya miaka
mingi, Na pia kuweza kumuhamisha katika level ya ku-hustle
ki-underground na kuwa Bonge la Star ndani na hata nje ya mipaka ya
Tanzania!
Kwa
hivi sasa, mbali na kuwa ndiye msanii anayependwa zaidi na mwenye
mashabiki wengi kuliko wote nchini, Diamond ndiye msanii anayeongoza kwa
kufanya shows nyingi nzuri na kulipwa pesa nyingi kuliko wote (almost 8
milions per show).. This is so wonderful!!!!
Katika kudhihirisha uwezo wake na nia njema aliyonayo juu ya industry hii
ya muziki wa bongo flava, Diamond ndiye msanii pekee aliyeweza kuajiri
vijana (madensa) na kuwalipa vizuri pamoja na kuishi nao kama ndugu,
kitu ambacho hakijawahi kufanywa na msanii yeyote tangu kuanza kupata
umaarufu kwa muziki huu wa bongo flava!
Kama hiyo haitoshi, Hivi sasa Diamond platnumz ameamua kupanua wigo wa ajira kwa Kuanzisha mchakato wa kutafuta washiriki rasmi kwa ajili ya video zake (video models) Kwa utaratibu wa kufanya Audience, lengo likiwa si wa kuwapa ajira tu, bali heshima wanayostahili tofauti na ilivyozoeleka kuwa ni wahuni tu wa kuokota mtaani!
Haya yote ni mageni lakini yanafaa kuigwa, Wasanii wa tasnia zote
nchini wanapaswa kuiga mfano wa DIAMOND wa kuwa wabunifu na kufikiria
mapinduzi ya kisanaa kwa ajili ya vizazi vijavyo na kuacha kuwa
wabinafsi..
No comments:
Post a Comment