LADIES:JE WAJUA WANAUME WANAWEZA KUWEKWA KIGANJANI BILA WAGANGA?
Mbinu chache za
kuwaweka waume zenu kiganjani.
Mpe mumeo anachohitaji :
Wanawake
wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa hisia na hata mawazo
ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka kwa wake zao hasa katika
masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue wanaume wengi wana hisia za haraka za
kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu
mfano mwanamke umevaa kanga moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua.
Wapo wanawake wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga
moja au night dress ndani huna kitu. Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa
mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia zake.
Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue tayari mwenzako
alishafiria mbali zamani we huna habari.
Ni vyema ukawa mwangalifu kujua
hisia za mwanaume huyo mumeo kama inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya
hivyo unamwathiri kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje
waliowaweka waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia. Akiwa na ahadi na
mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji atapewa
haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe hapewi je ana kosa
gani anapofikiria nje?
NB:
Nikisema mpe mumeo Hitaji lake sina maana
Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai si Mume
mwenye Busara huyo na wala hakutakii mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya
Tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Mvutie mumeo kwa mwenekano
wako:
Mvuto ni muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake
wanaowavutia kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi
yanayomvutia.
Sio vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga moja kama upo
pamoja nae. Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka kwa kuona. Kwanini
avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe unaweza kuvaa.
Wanawake jueni hili mnapokuwa karibu na waume zenu jianchieni Kwa mfano
hakuna ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini akiwa amechoka, wakati
unampotengea chakula ukavaa kanga moja au night dress. Unaweza kuona hilo ni
jambo dogo lakini kisaikolojia utakuwa umefanya jambo kubwa. Hapo hata kama
atakuwa ameudhiwa kazini atasahau na kukuona wewe mpenzi wake.
Usafi
panga vitu vyako vya chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa lizizungumzwa
sana hadi wengine wanasema mwanamke usafi. Kisaikolojia mpangalio wa vitu ndani
na hasa chumbani kama ni mbovu unaweza kuathiri hata tendo la ndoa. Kama chumba
ni kichafu vitu havijapangwa vizuri kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi
na hata kumfanya mwenzako achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani
hakupendi.
Mwanamke tandika kitanda chako vizuri panga chumba chako
tandika shuka nzuri. Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi nunua hiyo uwe
unatandika. Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe chumba chako na hata wewe
mwenyewe. Mazingira mazuri yatamfanya asisimke haraka kimapenzi anapokuwa na
wewe na hata kuitamana nyumba yake na kurudi mapema nyumbani.
Jinsi
chumba kilivyo rafu ndiyo wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata
kuchukia. Unaweza kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio
mbovu wa chumba ndio sababu inayomfanya achukie.
Uwe msafi wa
mwili:
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni
muhimu. Niwakumbushe wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama mwanamke
mchafu. Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi ukawa msafi. Oga
vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato kidogo yanayomvutia mumeo.
Sio lazima utumie gharama kubwa usafi wa kawaida unatosha na kupaka rotion kuna
fanya ngozi ya mwanamke ikawa laini inayovutia wanaume wanapenda sana wanawake
wenye ngozi laini yenye kuvutia inaleta msisimko mumeo anapokuwa anakuangalia
mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na
mengine ndiyo wanayotumia kuwaweka waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa
mganga hakuna atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi vitu
vyako vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo kufikiria
nje.
Kujiamini kwako iwe ni kwa sababu unajua ‘kumhendo’ mumeo kwa kumpa
mapenzi ya kiwango cha juu, kumheshimu, mjali na kumpatia mambo ya msingi ambayo
anastahili kuyapata kutoka kwako. Ukifanya hivyo utaifanya roho yake imsute kila
anapotaka kukusaliti.
Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe kujiamini na wala
huna sababu ya kujinadi kwa wenzako. Tambua kuwa kuna wanaofikia hatua ya
kuhatarisha maisha yao kwa kutoa ‘mtandao’ wakijua kuwa ni njia ya kuwashika
waume zao kumbe wanajitafutia matatizo makubwa.
Wapo waliopoteza fedha
zao nyingi kwa kwenda kwa waganga ili waume zao wasifurukute mbele zao lakini
imekuwa kazi bure. Shituka leo, anza kutumia mbinu sahihi za kuishikilia ndoa
yako na usijidanganye kwa kufanya mambo ambayo ni sawa na kutwanga maji kwenye
kinu.
Mwanamke aliyekamilika ni yule anayeuthamini mwili wake, sasa kwa
nini leo hii ukubali ‘kumrukisha ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje? Kwa nini
utumie fedha zako kwenye kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe mwenyewe ni
limbwata tosha?
No comments:
Post a Comment