Pia wamo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na
Dk Hussein Mwinyi na wa Nishati na Madini Sospeter
Muhongo.
Dar es Salaam. Ikiwa
imebaki miaka miwili kufanyika ka uchaguzi mkuu nchini, Kamati ya Vijana wapenda
Amani Tanzania, imetaja majina ya watu wanne wenye sifa za kuwania urais nchini,
huku ikieleza kuwa uzoefu wa miaka mingi si kipimo kizuri cha uongozi
bora.
Kamati hiyo imesema Watanzania wanatakiwa
kuwaogopa watu wanaojitaja wazi kuutaka urais, huku wakitumia majukwaa ya
kisiasa, kidini, kijamii, kiutamaduni na michezo kutoa misaada mbalimbali kwa
maelezo kuwa watu hao wakipewa nchi, wataongoza kwa maslahi ya kundi
fulani.
Waliotajwa katika orodha hiyo ni Mbunge wa
Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Hussein Mwinyi na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January
Makamba.
Katika orodha hiyo, kamati hiyo haikuwataja
viongozi waliowahi kujitangaza kutaka nafasi hiyo na ambao hawajajitangaza,
lakini wanaonekana kuwa na dhamira ya kugombea urais mwaka
2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Chifu Msopa, alisema wakati umefika kujadili mahitaji
ya nchi kiuongozi kwa manufaa ya siku zijazo,.
Katika maelezo yake, Msopa alitaja sifa za
kila kiongozi aliyemtaja katika orodha hiyo na kwamba kama ikitokea watu hao
wakashindwa kusimamishwa na vyama vyao kuwania urais mwaka 2015, kamati hiyo
itamuunga mkono yeyote ambaye atakuwa na sifa zinazofanana na watu hao
wanne.
Sifa za waliotajwa
Kwa upande wa ZittoMsopa alisema ana uwezo
mkubwa kiungozi, na kwamba mfano ni wa jinsi anavyosimamia Kamati ya Bunge ya
Mashirika ya Umma na kufichua madudu.
Kwa upande wa Mbatia, alisema kiongozi huyo
ni mzalendo wa nchi yake, ametulia na ana hekima kubwa ya kiuongozi na kwamba
busara zake zimedhihirika kwa jinsi anavyoongoza Kituo cha Demokrasia Tanzania
(TCD) kama mwenyekiti.
“Amekuwa akipigania ubora wa elimu ya watoto
wetu na kujali ujenzi wa taifa bora zaidi na ana uwezo wa kufanya kazi na
viongozi kutoka vyama vyote vya siasa.
Akitaja sifa za Makamba alisema wakati akiwa
mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini alikuwa msema kweli, jasiri kwa
kuikosoa Serikali inayoongozwa na chama chake.
Alisema Makamba wakati akiwa Wizara ya Mambo
ya Nje, alikuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka mitano na kufafanua
kuwa hiyo ni sifa ya muhimu kwa kiongozi.
Akimzungumzia Dk Mwinyi, Msopa alisema ana
busara na ndio sababu ya kuongoza vizuri wizara nyeti ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa.
No comments:
Post a Comment