Thursday, January 31

Wazanzibari mbaroni kwa biashara ya kununua wasichana TZ na kwenda kuwauza Uarabuni


Sakata la biashara ya binadamu ambalo limeibuka kwa kasi nchini limeanza kufanyiwa kazi na serikali baada ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Maji kuwatia mbaroni mawakala watano ambao ni wanawake wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, akizungumza na NIPASHE jana kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na jeshi hilo kukabiliana na tatizo hilo, alisema mawakala waliokamatwa ni wakazi wa Zanzibar na kwamba hatua za kisheria zimeanza

No comments:

Post a Comment

Search This Blog