Wednesday, April 17

Breaking News: Mwanamuziki mkongwe Bi Kidude afariki dunia



Taarifa zilizotufikia muda huu zinasema msanii mkongwe na mahiri katika fani ya muziki wa mwambao Fatuma binti Baraka almaarufu kama Bi Kidude amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Taarifa zilizothibitishwa na mwandishi wa habari wa ITV Farouk Karim zinasema kuwa Bi Kidude amefariki nyumbani kwake Bubu Zanzibar.

Bi Kidude aliwahi kusema hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya, ila inaaminika alikuwa na zaidi ya miaka 90.

Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Bi Kidude, Amen

No comments:

Post a Comment

Search This Blog