Thursday, April 18

SIKU YA MAZISHI YA BI. KIDUDE PAMOJA NA HISTORIA YAKE KWA UFUPI


Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia jana mchana  huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa leo. 

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....

Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.

Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
BAADHI YA SHOW ALIZOWAHI KUFANYA JIJINI DAR ES SALAAM. HII ILIKUWA June 30, 2012


Shabiki akimtunza Bi Kidude



Mashabiki wakipozi juu ya jukwaa ili kupiga picha na Bi Kidude.



Bi Kidude akionyesha umahili wake wa kucheza.
Hii ilikuwa usiku wa june 30 2011 katika ukumbi wa Equator uliopo Mtoni kwa Azizi Ally ambapo kulifanyika onyesho la taarab, wanamuziki mbalimbali wa taarabu waliudhuria akiwemo mwanamuziki mwalikwa toka Zanzibar Bi Kidude.
Baadhi ya bendi ambazo ziliudhuria onyesho hilo ni Five Star, TOT, East Africa Melod na Mashauzi Clasc



Baadhi ya picha enzi za uhai wake

Akitaniana na mtangazaji wa Clouds Tv, Sakina Lyoka


No comments:

Post a Comment

Search This Blog