Thursday, May 16

Kumbe Hip Hop Inauza Mwana Fa Apata Mil 18 kutoka Katika Miito ya Simu Ndani ya Miezi 18



Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.

Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.


Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.

No comments:

Post a Comment

Search This Blog