Jokate |
Jokate Mwegelo amabye ni actress, model, fashion designer, MC, Chanel O
presenter na mjasiriamali amesema kuwa licha ya kuachana na Hasheem
Thabit lakini bado anampenda kwakuwa ndiye mwanaume aliyeonyesha
kumjali. Jokate alionekana kumpa alama za juu Hasheem katika mapenzi
kuliko Diamond Platinumz na moja ya sababu ya kumwagana na Diamond ikiwa
ni mwanamuziki huyo kujitangaza katika media kwa kila demu anayetoka
nae kimapenzi kitu ambacho Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2 wa
mwaka 2006 hakukipenda. Akizungumza na GPL Jokate alisema "kugombana ni
sehemu ya mapenzi, ni kuonyesha kuwa mnapendana, ilitokea hivyo kwangu
kwasababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine, nahisi
hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani"
Jokate alipoulizwa kati ya Diamond na Hasheem ambaye ni mchezaji wa basketball nchini Marekani nani akimrudia atakubali alijibu kwa kusema "hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem" aliongeza kwa kusisitiza "yap...nilimpenda na ninampenda sana"
Jokate alisema kuwa uhusiano wake na Hsheem ulidumu kati ya miaka 2-3 wakati yeye na Diamond walidumu kwa miezi miwili pekee. Kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu kwasasa ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond kabla ya kumwaga na kuwa na yeye Jokate alisema "simchukii Wema, sina tatizo naye, unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara"
Jokate na Hasheem

No comments:
Post a Comment