Thursday, July 16

SABABU 8 UNA MAHUSIANO NA DEMU NA SIO MWANAMKE...


Wanawake na mademu ni vitu viwili tofauti kabisa, Wanawake wanaona dunia tofauti kabisa, na wanaichukulia tofauti ukilinganisha na mademu. Kuna mademu  kibao tena wa kumwaga ila kuna uhaba mkubwa wa wanawake na hili halina uhusiano wowote wa umri wao bali ni jinsi wanaivyoichukulia dunia.
Mademu au wasichana  huvaa nguo kuonyesha maungo yao wakiamini huwafanya wawe warembo zaidi wakati wanawake huvaa nguo yoyote ile wakiamini urembo upo pale pale.
Wanawake wanaelewa kuvaa nguo za kimitego sio njia pekee ya kuonekana mzuri.Mwanamke haitaji kuacha mambo yote hadharani ili watu wamuone kua n mzuri.Wanawake wanajiamini kutokana na walivyo na hawajali kitu wanachovaa sababu watazidi kua wazuri tu.
Lifestyle-mademu-wanajiachia-club
Mademu  hutegemea wanaume wao wajue wanavyojisikia bila kuwaambia kitu wakati wanawake huamini maogezi  kati ya wapenzi ni muhimu.
nyie mademu , wanaume hatuwezi kujua kitu mnachofikiria na tunatamani tungejua kwani ingefanya mambo kua marahisi sana lakini hatuwezi.wasichana wanaamini kua mwanaume inapaswa ajue kila kitu kuhusu wao kiasi cha kujua wanafikiri nii , wanahisi nini au wanamaanisha nini. Hii ndio inasababisha wasichana waanze fujo na majungu ambapo ingekua kwa mwanamke angejua kinachomsumbua na kuelezeaa.
Relationship-Demu-yupo-na-mshakaji
Mademu  hutegemea kulipiwa bili zao wakati wanawake wengi hujitegemea kwenye mambo mengi.
Wasichana au medemu hupenda kutuzwa kama watoto labda hii pia inaweza kuchangiwa na malezi.Kuna sababu sijui ni ipi inayowafanya mademu wasipende kutoa pesa kwenye pochi zao. Mwanamke hupenda kumkumbusha mpenzi wake kwamba amempenda sababu anamheshimu na kumjali na sio kwasababu ya pesa zake.
Relationship-jamaa-analipa-dinner-date
Mademu  hunywa na  kulewa na wanawake hunywa kufurahia au ku-relax
Je unamjua mwanamke anayekunywa hadi kuanza kuyumbayumba ? of course , haumjui. Mwanamke hawezi kufanya hivyo. Mademu  ndio wanatabia hizo na hii husababisha kufanya maamuzi yasiyo sahihi.
Relationship-demu-anakunywa-bia-balaa
Mademu  hawakawii  ku-update  Facebook status to “In a relationship” – wakati wanawake hata huo muda wa Facebook hawana.
Kawaida wanawake wako busy sana na  maisha hasilia kiasi kwamba hawana muda kwa ku-update status facebook.  Wanaweza kufanya hivyo kama wapo kwenye mtandao na kukumbuka lakini hawawezi kukimbia facebook ili tu ku-update status.
Relationship-demu-yupo-facebook
Mademu wanaangalia Vipindi vya kijinga Wanawake wanasoma
kwa kawaida vipindi vya TV au videos kwenye internet ni nzuri sema sehemu kubwa imejaa vitu vya kijinga. Wanawake wana vipindi vyao pia ambapo mara nyingine hupenda kuangalia wakiwa wanasoma gazeti au kitabu. Kama wewe una demu ukimwekea taarifa ya habari anakimbia basi jiulize mara mbili mbili..
Relationships-Demu-anaangalia-TV
Mademu wanaongea pumba huku wanawake wakiwa na ufahamu wa mambo
Hii ni moja ya kitu kikubwa kinachomtenganisha msichana na mwanamke.Mademu wengi wanazingua inapokuja swala la kuzungumzia vitu vya msingi vinavyoizunguka jamii.Mademu hua hawana vitu vya kielimu ambavyo wanaweza kufanya na ku-enjoy na mtazamo wao kawaida sio kutoka kwao bali kwa watu  wengine ambapo wamesikia na kuufanya wa kwao.
Relationships-Mademu-wambeya
demu anataka kuendeshwa bali mwanamke haitaji  mtu yoyote bali yeye mwenyewe
Hakuna kitu kinachovutia kwenye mapenzi kama mwanamke anayeweza kujiendesha mwenyewe.Wanawake hupata kitu wanachotaka na hawaitaji mtu yoyote kuwaongoza.
Relationship-wapenzi-wanachuniana-kitandani

1 comment:

Search This Blog