Thursday, July 16

Ukiona dalili hizi, jua kua hupendwi !!!


Siyo kitu rahisi kuelewa kile kinachoendelea akilini mwa mwanamke,watu wengi wanahamu ya kujua kila anachowaza mpenzi wake,labda kama amechoshwa mahusiano yenu,au tu labda hataki yeye kuwa wa kwanaza kukumwaga.Mara nyingi huwa anaonyesha dalili hizi na kama u kilaza sana kusoma katikati ya mistari,basi mwisho wa siku ataamua tu kukwambia ukweli na kuachana na wewe.Hizi ndizo zile dalili tano  kujua kuwa mpenzi  wako amepoteza mapenzi aliyokuwa nayo kwako.

Anapunguza kukupigia au kukutumia ujumbe wa maneno.
Fikiria hiki,Wanawake wengi wanapenda kuongea,kwa mwanamke akupendaye ndiyo atazidisha kasi ya kuongea na wewe,hata kama amekasirika na hataki kuongea na wewe,ataendelea kusisitizia kuwa hataki kuongea na wewe.Hamna kitu kinachomfanya mwanamke anyamaze pale anapojiskia kuongea na wewe kwa hiyo ukiona kuwa amepunguza ile spidi ya kuongea na wewe ,kukupigia simu au kukutumia messeji ujue hapo kuna kitu.Tena usishangae pale unapomtext alafu anakujibu kwa kwa kutumia herufi” K” akimaanisha “Okey”ujue hapo unam’boa,hana interest na wewe.
Relationships-upungufu
Hakuonyeshi tena hisia zake kama zamani.
Kwa mwanamke ameumbwa na roho ya kujali,kama mpenzi wako ameacha kukupigia kelele unapofanya jambo,kuna mawili labda hajali tena kwa chochote unachomfanyia ua amehifadhi  maudhi yote ili siku yakimshinda akulipukie na kukwambia kinachomkera pale uvumilivu utakapomshinda,yote haya ni dalili kuwa mpenzi wako amekuchoka.Mara nyingi inabidi kulinganisha utofauti wa hisia za mpenzi wako haswa anapo-react juu ya baadhi ya mambo ,utofauti wakati ulipoana mapenzi yenu na hivi sasa,ukiona amekuwa mpole sana na hajali tena kama zamani,ujue hapo umempoteza.
lifestyle-wapenzi-hawana-muda
Mabadiliko yake pale mnapokuwa pamoja.
Hii ni moja ya vitu muhimu vya kuangalia pia kwa mpenzi wako,akijaribu kukuzuia hata pale unapotaka kumkumbatia mnapokuwa pamoja na hata hadharani ,ujue mapenzi yamepungua.Kama hafanyi yale yote aliyokuwa anapenda kuyafanya mnapokuwa pamoja ,ujue kuna tatizo,kama mlikuwa mnapenda kufanya jambo flani wote alafu,ghafla tu unahisi mpenzi wako ,hafurahii tena kama zamani,ujue hiyo ni dalili kuwa hakuna mapenzi tena.
Wapenzi-kitandani
Wivu umepungua.
Wanaweza kukataa ila wanawake wameumbwa na wivu,tena hakuna mwanamke ambaye anapenda ku-share mpenzi wake na mwanamke mwingine,kwa hiyo atafanya kila awezacho ili akufanye uwe na furaha,ili uwe unamfikiria na kumuwaza yeye tu.Ukiona pale mpenzi wako ameacha kuwa na wivu,yuko poa kwa kila ufanyacho,labda hajali hata ukimwambia kuwa upo na rafiki yako, na bado akisikia sauti za wanawake asikuletee utata,au asikuulize maswali kama hao ni wakina nani,au kutoonyesha dalili zozote za kuwa na wivu,ujue kuwa hapo hakuna mapenzi tena.
mapenzi-motomoto
Hatambui tena hisia zako.
Wanasema wanawake ndio viumbe wadadisi sana,na ni vigumu kuwaficha kitu,unaweza kuficha kwa muda ila mwisho wa siku atagundua tu.Kwa mwanamke akupendae ni rahisi sana kusoma hisia zako haswa pale aonapo kitu kinapokwenda vibaya,mara nyingi huuliza nini tatizo au kujaribu kukufanya usahau,kwa kukuchekesha hivi  au chochote kile awezacho kufanya.Ukiona kuwa mpenzi wako hajali,hata kama umerudi kazini hawezi kuona hata kama,umechoka na hata hakuulizi,ujue napo hapo amepoteza mapenzi kwako.
lifestyle-anatoswa-yupo-busy-mpenzi

No comments:

Post a Comment

Search This Blog