Thursday, July 16

SABABU ZINAZO PELEKEA WATU KUPENDELEA KUWA SINGLE....

Katika maisha ya kawaida imezoeleka kuona watu wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na hatimaye wengine kufikia hadi kufunga ndoa ila kunawengine hawatekelezi hata kimoja kati ya hivyo. Hii inaweza kuchangiwa na sababu mbali mbali ambazo zinaweza kuwa kikwazo ama wengine kupendelea hivyo. Takwimu zinaonyesha kuwa kadiri ya siku zinavyokwenda ndivyo idadi hii inaongezeka kutokana na mabadiliko yanayoweza kuwa ya kiuchumi ama ya kijamii kiujumla. Baadhi ya sababu hizo zinaweza kua;


Ugumu wa maisha
Kutokana na jinsi ilivyozoeleka katika jamii kuwa mwanaume ndio mtafutaji, sasa na jinsi hali ya maisha inavyozidi kupanda ndipo inapompelekea na yeye kufanya kazi zaidi ili aweze kwenda nayo sawa huku akijikimu na mahitaji yake. Hali hii inaweza kumfanya awe anafanya kazi muda wote kupelekea mpaka kukosa mda wa mahusiano au hata akiwa kwenye mahusiano inakuwa kuonekana ni vigumu sana kutokana na mihangaiko. Hii inaweza kuchangia pia mtu kutotaka kuwa kwenye mahusiano.

Uhuru wa mtu binafsi
Kila binadamu huwa anapendezwa na uhuru wake yeye binafsi na kuweza kufanya mambo yake bila kushurutishwa na mtu. Sasa kutokana na uhuru huo, kuna wengine wanauchukulia kivingine na kuwa wabinafsi kwa kumaanisha kwamba  anakua hayupo tayari kujitoa na mwenzake,kumjali au kutaka kujenga maisha na mwenzake akiamini kuwa itamrudisha nyuma kimaendeleo, bado anataka kuendelea kujenga  maisha yake. Hii inaweza ikawa kichocheo pia cha kufanya watu kutotaka kuwa kwenye mahusiano.

Kujiongeza kielimu
Ni vizuri sana kupenda kuongeza elimu ili kuwa na ufahamu mkubwa katika mambo mbali mbali na hata kusaidia jamii yako kutokana na elimu uliyoipata. Ila wakati mwengine elimu isizidi maarifa kwa kuwa Utakuta watu wengine wanakua na hamu ya kuendelea na elimu huku wakisahau kabisa kuhusu maisha ya kijamii yani kuwa na mahusiano,kujichanganya na watu au kutaka kuanzisha familia. Kama unavyojua elimu huwa haina mwisho kwa kuwa vitu vipya vinatoka kadiri kila mara ambavyo vinahitaji uelewa wetu. Usipoangalia unaeza ukajikuta umri umekwenda na bado upo peke yako bila na matumaini ya kuwa na mwenza wala ya kuanza familia.

Kuvunjika kwa mahusiano
Hii naweza kusema kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha watu kutaka kubaki peke yao bila kuwa na mahusiano kama ya ndoa ama ya kawaida kutokana na maumivu waliyoyapata  na uhusiano waliotoka. Watu wengi huwa wanaishi kwa kusonga mbele huku wakizingatia kule walipotokea  ili kuhakikisha yasijirudie makosa. Utakuta mtu hataki tena kuwa kwenye ahusiano kwa kuwa anakumbuka shida,tabu, manyanyaso ama kutokua huru. Kwa kuwa ameshaonja chachu hiyo, wengi huwa wanakua hawapo tayari kurudi tena katika hali hiyo, anaona bora abaki mwenyewe.

Kutokua na uwezo wa kujitoa kwa mwenzako
Kuna watu wengine wanakuwa hawapo tayari kujitoa kwa hisia kwa mwenza wake yani anakua mgumu kwa kila kitu hasa tukiangalia kwa upande wa fedha. Wanaume wengi wamekuwa wakiogopa kujiingiza katika ndoa kwa kuwa wanafikiria siku atakapo achana nae atalazimika kugawana nae mali. Hii huwa ni fikra mbaya ambayo pia huchochea kwa namna kubwa sana wao kubaki peke yao na kutojihusisha kwenye mahusiano.

UNAPASWA KUJUA MAMBO HAYA SABA KUHUSU MWANAMKE...

1)Anapenda kupungua uzito na pia wakati huo huo ni vigumu kuacha tabia ya kula vyakula vya sukari vinavyomuongezea uzito.

kupunua-uzito
2)Anapretend kuwa hapendi sex, ndio! ila ukweli ni kwamba kila binadamu awe wakiume au wakike, ambaye hapendi ku-do, labda awe mgonjwa au ameshawahi kupatwa na matatizo yakisaikolojia.
hataki-kufanya-mapenzi
3)Anaweza kusema hakupendi, ila anashindwa kujizuia kukufikiria kila siku.
asante wapenzi
4)Katikati ya mwezi unapomkaribisha nyumbani anaweza akatae, ila ikifika mwisho wa mwezi anakuwa mtu wa kwanza kukumbusha kuchukua mshahara wako na kupanga ratiba ya jinsi ya kuitumia.
kachunwa-pesa
5)Siku zote anaweza kukwambia umuongezee vocha kwenye simu yake na utashangaa hadi hela inaisha unaishiwa kubipiwa kila siku ili upige.
anataka-vocha
6)Anakuwa wa kwanza kulia pale utakapomkosea, ila akikukosea huanza kucheka na ku-smile.
demu-analia
7)Kukwambia we ni mbaya, kwake ni utani, ila unapomwambia yeye m’baya, anaweza asikusamehe maishani mwake.
wanabishana-wapenzi

SIRI 9 ZA KUWANA UHUSIANO IMARA.....

09. Kuelezea Hisia

Moja kati ya msingi wa kuwa na mahusiano imara ni uwezo wa kuonesha hisia zako kwa parter wako na kujua kumsikiliza.kusema “nimekuelewa” haimaanishi “nimekubaliana na wewe” hivyo ni vema kumsikiliza mwenzio kuliko kukubali kila kitu ilimradi kuwe na amani.
relationship-wapenzi-wanacheza-game
08 . Panga Quality time na partner wako
Hasa uhusiano unapozidi kukua ni muhimu kuwa na muda wa pekee ambao mtazungumza kuhusu uhusiano wenu pekee na mipango muhimu ya baadae.
Relationships-wapenzi-wanakula
07. Bishaneni lakini kwa jambo maalumu
ule mpango wa kukusanya malalamiko kibao ya mwezi wako mfano pale mnapogombana kuhusu kuchelewa on a date then mnaanza kuongezea na vitu vingine kibao kama kutompigia simu , kutovaa vizuri , kutokujali na mengine kibao.Kubishana kuhusu mambo mia kwa wakati mmoja ni vigumu kukabiliana nako hivyo bishaneni mara moja jambo linapotokea.
Relationships-wanabishana-wapenzi
06. Ongeza vitu vipya katika mahusiana
Ile safari ya kwenda wote kwa mara ya kwanza zanzibar au kujifunza kozi mpya basi ni vyema kuvifnya vitu hivi vipya pamoja. Ni vyema kukua pamoja  , na kupeana changamoto pamoja mkiwa na uzoefu mpya mlioupata pamoja.
Relationships-black-coupl-zanzibar
05. Onesha Shukrani
kila mtu hapendi kuonekana yupo chini lakini kumshukuru mwenzako kwa safari aliokupeleka mbuga za wanyama au pesa za matumizi alizokupa kutamfanya asione kwamba unamchukulia poa na kutamfanya aendelee kukudhamini na kukuzidishia mambo mazuri.
Relationships-asante-wapenzi
04. Omba ruhusa kuongelea jambo fulani
Simaanishi uombe kwa unyonge bali pale unapotaka kuzungumza na mwezako kuhusu jambo lilalogusa sana maisha yenu ni vizuri kuuliza kwanza kama ni wakati sahihi.
Relationships-mpenzi-omba-ruhusa-kuongea
03. Msisahau Mlianzaje
kumbukeni mlivyoanza , jinsi mapenzi yalivokua , hata kama mmeishi kwa miaka mitano pamoja msiache zile hisia za mwanzo zikaondoka. Fanya juhudi za kuwa mbunifu na mshangaze mwezio.
Relationship-wachumba-kwa-kitanda
02. kukua
kukua na kubadilika kama wewe  kutafanya mahusiano yenu kuwa bora zaidi. Moja ya vitu muhimu kabisa katika mahusiano ni kujifunza kuhusiano na wewe mwenyewe zaidi au sawa na utakavyojifunza kuhusu partner wako. Kwa kuangalia vitu unavyofanya ukiwa na partner wako na jinsi anavyokuletea changamoto itakufanya na wewe ukue kilazima.
Relationship wachumba-wanahug
01. Usiwaache Rafiki zako
Ni dhahiri kwamba unataka mchumba wako ndio awe wa kwanza kupata habari nzuri pale inapotokea au mtu wa kwanza kufuta machozi yako pale unapopata shida lakini mara nyingine utamuhitaji rafiki yako hasa kwa wanawake kuna vitu ukimwambie  mchumba wako hawezi kukuelewa lakini ukijadiliana na rafiki yako wa kike anaweza kukusaidia na kukupa ushauri.
relationship-rafiki-wa-kike

UKIONA MWANAMKE ANATABIA HIZI BASI UJUE NI KICHECHE....

Anamarafiki wakiume kwa faida.

Kwa mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo ishu, ila ishu ni pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume, na kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale, ila kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo cheche.
Lifestyle-wanaume

Anakasirika haraka usipompa anachotaka.
Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe week nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.
Lifestyle-demu-anataka
Siyo rahisi kupenda.
Wanawake vicheche huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano, wanataka siku zote wawe available ili kwa mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye, na hata akiamua kupenda, huwa hakai sana, labda kama unamsaidia asilimia 90% ya matatizo yake.
Lifestyle-demu-kicheche
Anachukulia mahusiano kama biashara.
Watu kama hawa huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako.
lifestyle-demu-anataka-zawadi
Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo.
Kwa mwanamke kicheche, pale tu utapomchekea na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka.
lifestyle-demu-anategeka

Ukiona dalili hizi, jua kua hupendwi !!!


Siyo kitu rahisi kuelewa kile kinachoendelea akilini mwa mwanamke,watu wengi wanahamu ya kujua kila anachowaza mpenzi wake,labda kama amechoshwa mahusiano yenu,au tu labda hataki yeye kuwa wa kwanaza kukumwaga.Mara nyingi huwa anaonyesha dalili hizi na kama u kilaza sana kusoma katikati ya mistari,basi mwisho wa siku ataamua tu kukwambia ukweli na kuachana na wewe.Hizi ndizo zile dalili tano  kujua kuwa mpenzi  wako amepoteza mapenzi aliyokuwa nayo kwako.

Anapunguza kukupigia au kukutumia ujumbe wa maneno.
Fikiria hiki,Wanawake wengi wanapenda kuongea,kwa mwanamke akupendaye ndiyo atazidisha kasi ya kuongea na wewe,hata kama amekasirika na hataki kuongea na wewe,ataendelea kusisitizia kuwa hataki kuongea na wewe.Hamna kitu kinachomfanya mwanamke anyamaze pale anapojiskia kuongea na wewe kwa hiyo ukiona kuwa amepunguza ile spidi ya kuongea na wewe ,kukupigia simu au kukutumia messeji ujue hapo kuna kitu.Tena usishangae pale unapomtext alafu anakujibu kwa kwa kutumia herufi” K” akimaanisha “Okey”ujue hapo unam’boa,hana interest na wewe.
Relationships-upungufu
Hakuonyeshi tena hisia zake kama zamani.
Kwa mwanamke ameumbwa na roho ya kujali,kama mpenzi wako ameacha kukupigia kelele unapofanya jambo,kuna mawili labda hajali tena kwa chochote unachomfanyia ua amehifadhi  maudhi yote ili siku yakimshinda akulipukie na kukwambia kinachomkera pale uvumilivu utakapomshinda,yote haya ni dalili kuwa mpenzi wako amekuchoka.Mara nyingi inabidi kulinganisha utofauti wa hisia za mpenzi wako haswa anapo-react juu ya baadhi ya mambo ,utofauti wakati ulipoana mapenzi yenu na hivi sasa,ukiona amekuwa mpole sana na hajali tena kama zamani,ujue hapo umempoteza.
lifestyle-wapenzi-hawana-muda
Mabadiliko yake pale mnapokuwa pamoja.
Hii ni moja ya vitu muhimu vya kuangalia pia kwa mpenzi wako,akijaribu kukuzuia hata pale unapotaka kumkumbatia mnapokuwa pamoja na hata hadharani ,ujue mapenzi yamepungua.Kama hafanyi yale yote aliyokuwa anapenda kuyafanya mnapokuwa pamoja ,ujue kuna tatizo,kama mlikuwa mnapenda kufanya jambo flani wote alafu,ghafla tu unahisi mpenzi wako ,hafurahii tena kama zamani,ujue hiyo ni dalili kuwa hakuna mapenzi tena.
Wapenzi-kitandani
Wivu umepungua.
Wanaweza kukataa ila wanawake wameumbwa na wivu,tena hakuna mwanamke ambaye anapenda ku-share mpenzi wake na mwanamke mwingine,kwa hiyo atafanya kila awezacho ili akufanye uwe na furaha,ili uwe unamfikiria na kumuwaza yeye tu.Ukiona pale mpenzi wako ameacha kuwa na wivu,yuko poa kwa kila ufanyacho,labda hajali hata ukimwambia kuwa upo na rafiki yako, na bado akisikia sauti za wanawake asikuletee utata,au asikuulize maswali kama hao ni wakina nani,au kutoonyesha dalili zozote za kuwa na wivu,ujue kuwa hapo hakuna mapenzi tena.
mapenzi-motomoto
Hatambui tena hisia zako.
Wanasema wanawake ndio viumbe wadadisi sana,na ni vigumu kuwaficha kitu,unaweza kuficha kwa muda ila mwisho wa siku atagundua tu.Kwa mwanamke akupendae ni rahisi sana kusoma hisia zako haswa pale aonapo kitu kinapokwenda vibaya,mara nyingi huuliza nini tatizo au kujaribu kukufanya usahau,kwa kukuchekesha hivi  au chochote kile awezacho kufanya.Ukiona kuwa mpenzi wako hajali,hata kama umerudi kazini hawezi kuona hata kama,umechoka na hata hakuulizi,ujue napo hapo amepoteza mapenzi kwako.
lifestyle-anatoswa-yupo-busy-mpenzi

SABABU 8 UNA MAHUSIANO NA DEMU NA SIO MWANAMKE...


Wanawake na mademu ni vitu viwili tofauti kabisa, Wanawake wanaona dunia tofauti kabisa, na wanaichukulia tofauti ukilinganisha na mademu. Kuna mademu  kibao tena wa kumwaga ila kuna uhaba mkubwa wa wanawake na hili halina uhusiano wowote wa umri wao bali ni jinsi wanaivyoichukulia dunia.
Mademu au wasichana  huvaa nguo kuonyesha maungo yao wakiamini huwafanya wawe warembo zaidi wakati wanawake huvaa nguo yoyote ile wakiamini urembo upo pale pale.
Wanawake wanaelewa kuvaa nguo za kimitego sio njia pekee ya kuonekana mzuri.Mwanamke haitaji kuacha mambo yote hadharani ili watu wamuone kua n mzuri.Wanawake wanajiamini kutokana na walivyo na hawajali kitu wanachovaa sababu watazidi kua wazuri tu.
Lifestyle-mademu-wanajiachia-club
Mademu  hutegemea wanaume wao wajue wanavyojisikia bila kuwaambia kitu wakati wanawake huamini maogezi  kati ya wapenzi ni muhimu.
nyie mademu , wanaume hatuwezi kujua kitu mnachofikiria na tunatamani tungejua kwani ingefanya mambo kua marahisi sana lakini hatuwezi.wasichana wanaamini kua mwanaume inapaswa ajue kila kitu kuhusu wao kiasi cha kujua wanafikiri nii , wanahisi nini au wanamaanisha nini. Hii ndio inasababisha wasichana waanze fujo na majungu ambapo ingekua kwa mwanamke angejua kinachomsumbua na kuelezeaa.
Relationship-Demu-yupo-na-mshakaji
Mademu  hutegemea kulipiwa bili zao wakati wanawake wengi hujitegemea kwenye mambo mengi.
Wasichana au medemu hupenda kutuzwa kama watoto labda hii pia inaweza kuchangiwa na malezi.Kuna sababu sijui ni ipi inayowafanya mademu wasipende kutoa pesa kwenye pochi zao. Mwanamke hupenda kumkumbusha mpenzi wake kwamba amempenda sababu anamheshimu na kumjali na sio kwasababu ya pesa zake.
Relationship-jamaa-analipa-dinner-date
Mademu  hunywa na  kulewa na wanawake hunywa kufurahia au ku-relax
Je unamjua mwanamke anayekunywa hadi kuanza kuyumbayumba ? of course , haumjui. Mwanamke hawezi kufanya hivyo. Mademu  ndio wanatabia hizo na hii husababisha kufanya maamuzi yasiyo sahihi.
Relationship-demu-anakunywa-bia-balaa
Mademu  hawakawii  ku-update  Facebook status to “In a relationship” – wakati wanawake hata huo muda wa Facebook hawana.
Kawaida wanawake wako busy sana na  maisha hasilia kiasi kwamba hawana muda kwa ku-update status facebook.  Wanaweza kufanya hivyo kama wapo kwenye mtandao na kukumbuka lakini hawawezi kukimbia facebook ili tu ku-update status.
Relationship-demu-yupo-facebook
Mademu wanaangalia Vipindi vya kijinga Wanawake wanasoma
kwa kawaida vipindi vya TV au videos kwenye internet ni nzuri sema sehemu kubwa imejaa vitu vya kijinga. Wanawake wana vipindi vyao pia ambapo mara nyingine hupenda kuangalia wakiwa wanasoma gazeti au kitabu. Kama wewe una demu ukimwekea taarifa ya habari anakimbia basi jiulize mara mbili mbili..
Relationships-Demu-anaangalia-TV
Mademu wanaongea pumba huku wanawake wakiwa na ufahamu wa mambo
Hii ni moja ya kitu kikubwa kinachomtenganisha msichana na mwanamke.Mademu wengi wanazingua inapokuja swala la kuzungumzia vitu vya msingi vinavyoizunguka jamii.Mademu hua hawana vitu vya kielimu ambavyo wanaweza kufanya na ku-enjoy na mtazamo wao kawaida sio kutoka kwao bali kwa watu  wengine ambapo wamesikia na kuufanya wa kwao.
Relationships-Mademu-wambeya
demu anataka kuendeshwa bali mwanamke haitaji  mtu yoyote bali yeye mwenyewe
Hakuna kitu kinachovutia kwenye mapenzi kama mwanamke anayeweza kujiendesha mwenyewe.Wanawake hupata kitu wanachotaka na hawaitaji mtu yoyote kuwaongoza.
Relationship-wapenzi-wanachuniana-kitandani

JE, UNATAKA KUISHI KWA FURAHA NA MPENZI WAKO?

je, Unataka kuishi kwa furaha na mpenzi wako ?

Katika mahusiano ya wanandoa, wapenzi au wanaoishi pamoja yanaweza kudumishwa kutokana na upendo uliojengwa kwa misingi ambayo inabidi ifwatishwe ili kufikia lengo. Mahusiano huwa yanatofautiana kwa jinsi kila mtu anavyoyachukulia kwa maana hiyo hamna sheria kuu ya kuyaongoza bali huwa kuna muongozo ambao japo unakuonesha njia sahihi ya kuweza  kuwafanya mfike mbali na muwe na  furaha.
Muongozo huu umejengwa ama umetokana na mikasa ya maisha ya kila siku iliyotokea  kwa  wenye mahusiano ili isipate kujirudia hali ya kutokuwa na maelewano wala furaha. Muongozo huo ama sababu hizo ni kama;

Kuachana isiwe suluisho la kwanza
Ukiuliza sehemu mbali mbali kuhusu njia gani ya kusuluhisha matatizo kwa wapenzi ama wanandoa utasikia “acha nae tafuta mwengine”, hili ni kosa kubwa sana kwa kuwa utakuta mtu anaingia kwenye mahusiano au ndoa huku akilini kashaweka  kuwa ukizingua muda wowote naweza kukuacha. Mahusiano haya hayawezi kudumu muda mrefu kwa kuwa kila mmoja takuwa anatafutia sababu mwenza wake pindi pale wanapokorofishana ili aweze kujitoa badala ya kujaribu kulitatua tatizo. Inabidi   uwe makini na upige moyo konde ukidhamiria kusuluhisha ili nyote muwe na furaha ya kweli.
Relationship-wapenzi-wanagombana-kitandani

Mahusiano yaendane na kila aina ya hali
Hamna mtu anayeweza kusema kuwa mahusiano yake yamekamilika kwa kuwa  mapungufu hayakosekani. Unaweza ukasema furaha ipo katika mahusiano yenu kwa kuwa labda kipato chenu ni kizuri kwa wakati huo ila hali ikibadilika inaweza ikawa chachu ama sumu ya kuharibu mahusiano yenu kwa kuwa labda mmoja wenu hajazoe kuishi katika hali duni. Katika maisha kuna kupanda na kushuka, hivyo basi hamna budi kuvumiliana kwa shida na raha. Watu walio kwenye mahusiano wakiweza kubalance nyakati za shida na raha hao ndio wanaweza kuwa na mahusiano yenye furaha siku zote na uhusiano wao ukadumu zaidi.
Relationships-mpenzi-omba-ruhusa-kuongea

Usijenge hofu kwa mwenzako ama kwake pia
Sababu nyingine ya kuwa kwenye mahusiano yenye furaha ni kuwa muwazi kwa mwenza wako . Kuwa huru kujielezea kwa mwenzako na wakati huo huo mfanye mwenzako asiwe na uwoga wa kukueleza jambo lolote kiuwazi akihofia malumbano.  Mara nyingine mkielezana jambo linalowatatiza kwa muda huo linaweza kuisha kiurahisi kuliko hata mlivyotegemea ila ukiweka duku duku  na ukikaa kimya bila kuzungumza na mwenza jambo linaweza likakuwa kubwa siku nyingine ikawa shida kusuluhisha.Hii inaondoa dhana ya nidhamu ya uwoga, hata mwenzako akikosea inakuwa rahisi kumwambia ili ajirekebishe na mambo yaweze kuendelea bila matatizo yoyote.
relationship-nataka-space

Kumuheshimu,kumjali na kumpenda kwa vitendo mwenza wako
Mara nyingi siku hizi imekuwa rahisi sana kumwambia mwenza wako neno “nakupenda” ila upendo wako unakuwa hauambatani na vitendo vinavyoendana na hali hiyo. Neno “upendo” hua haliji peke yake bali huwa linakuja na furushi la mambo yanayofanya neno lenyewe likamilike. Mambo yenyewe ni kama heshima, kujali, kushirikishana, kujitoa kwake kwa hali mali na kusameheana pindi mmoja anapoteleza au kukosea. Onyesha hisia zako za kweli kwa mwenza wako ili aweze tambua uzito wa upendo wako kwake. Ukizingatia hayo basi bila shaka utakua na furaha kwenye mahusiano.
Relationships-kamilifu

Muwe kitu kimoja siku zote
Hata siku moja usije jaribu kutokuwa upande wa mwenza wako ama kutomuunga mkono kwenye mambo mbali mbali. Kwenye jambo jema muunge mkono na uzidi kumpa moyo na kwenye jambo ambalo unaona litakuwa baya kwake usimwache hivi hivi bali mshauri ili aweze fikia shauri jema. Kama mkiwa wenyewe kwenye mazingira ya peke yenu mnalumbana kuhusu mjadala flani  mpaka ikafikia hatua ya kukubaliana ama kutokubaliana basi iwe  ni kati yenu lakini mkiwa mpo kwenye umati wa watu wote muwe na sauti moja kuhusu mjadala huo. Hii huwa inasaidia sana kuimarisha mahusiano yenu  ukizingatia kama mmoja wenu mjadala huo mlimvunja moyo na kumfanya asiwe na raha mbele za watu. Kuwa na msimamo mmoja pia itaonyesha jinsi gani nyinyi nyote jinsi gani upendo wenu ulivyoshiba na pia furaha lazima itapata chimbuko la kutokea.
Relationships date


KINGUNGE: MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM ULIKUWA BATILI



JANA Mzee Kingunge kaongea na vyombo vya habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi…

CHACHANDU NA MAANA YAKE KATIKA ULIMWENGU WA MAHABA


Asalam alaikum/ Bwana Yesu asifiwe mashosti zangu? Leo katika kolamu yetu ya kicheni pati tunakuletea maana nzima ya chachandu katika mapenzi kwani kuna watu wengi hawajui na wamekuwa wakiuliza.

Shosti asikwambie mtu kwa wanaume wengi wa Kiafrika wanapenda sana mwanamke kuwa na chachandu kwani wanakwambia zinawapa raha na utulivu wanapokuwa faragha.
Wanapata vipi? Wanajua wao, lakini baada ya mada hii kufika tamati najua nitapata ujumbe mwingi ukieleza jinsi gani wanafurahika.
Leo ni wengi wanataka kujua zinavaliwa wakati gani, shosti si kila sehemu unavaa chachandu angalia na sehemu ya kuzivaa kwa sababu ukizivaa eneo la kazi utatafsiriwa vibaya, zile zinafaa kuvaliwa chumbani ukiwa na mpenzi wako tu.
Unajua zile zinatungwa na uzi huenda ukazivaa na ikatokea zikakatika hivi utajisikiaje ukiwa sokoni halafu zikakatika lazima utaona aibu na wengine hudiriki kuziacha hapohapo.
Cha kufanya shosti yangu vaa kwa raha zako wakati unahisi mumeo anataka kurudi nyumbani, ukishaoga na umeshajiandaa kwa kumpokea mume unaweza kuvaa chachandu kwani zitachangia kumuweka tayari mumeo.
Sasa basi zifahamu hasa maana za rangi ya chachandu hizi na kazi yake.
Ukiachia mbali kunakshi kiuno chako pia zinamaana kwa rangi mojamoja ingawa siku hizi wanawake wamekuwa wakichanganya rangi kwa ajili ya mapambo tu na kumvutia mume lakini kuna rangi ambazo ni viashirio vya lugha ya kuwasiliana na mwenzako pale utakapotaka abaini jambo fulani na maana hizi ndiyo nakuletea shoga yangu.
Rangi kama pinki, bluu, dhahabu: hizi rangi hazina maana kwenye sita kwa sita ni urembo tu kupendezesha kiuno, hukatazwi kuzivaa shosti sasa ninazokufundisha ni hizi.
Nyekundu: Ukimkuta mwanamke amevaa chachandu ya rangi hii unatakiwa kuelewa kwamba mwanamke huyu yupo kwenye hedhi, kwahiyo wewe fanya mengine lakini siyo safari ya kupeana maraha kwani kwa kufanya hivyo kiafya si vizuri unatakiwa kuwa mpole tu.
Nyeupe: Ukimkuta mwanamke amevaa chachandu nyeupe hii humaanisha hana tatizo lolote litakalomfanya asikupe raha ya sita kwa sita, kwa hiyo ukitaka tu muda wowote unapata kwani anakuwa amejipanga kwa lolote.
Nyeusi: Ukimkuta mwanamke amevaa rangi hiyo, humaanisha ya kwamba yupo tayari kukupa raha za sita kwa sita lakini uwanja wake haujakatwa majani, kwa hiyo chaguo ni lako kama unataka kutumia siku nzima kutafuta goli haya, ama kama utamsaidia kumkatia majani uwanjani vizuri zaidi ama kama huwezi yote basi mpe muda akate mwenyewe.
Wanawake wa zamani walikuwa hawavai chachandu, wanatandika sita kwa sita vizuri kisha wanatupia langi wanayoona inamfaa kwa siku hiyo, baba akitoka safari anakuta chachandu ya rangi nyekundu iko kitandani anajua mkewe alikuwa anatumikia siku zake siku zinaenda.
Mashosti kuna wengine hawapendi kuvaa kabisa unaweza kutumia kwa kuitupia ile unayoona inakufaa kumfikishia ujumbe mume wako kwa siku hiyo, lakini kumbuka kwa kuivaa inaleta hamasa fulani na kukusaidia kumuweka karibu mumeo.
Wapenzi mashosti zangu, kwa leo naomba niishie hapa ila panapo majaliwa tutaonana tena siku yingine.

Ushauri: Nilizaa na dada yangu, Je nitapata laana?




Mpekuzi habari za kuhaingaika, 

Kwetu tumezaliwa wawili tu mapacha , Mimi na Dada yangu, baba yetu alikua mkali na mkoloni sana hatukuruhusiwa kutoka nje kabisa labda shule tu na tulienda na Gari la nyumbani Tulikua tukiishi mkoani na ilikua ni mwishoni mwa miaka ya tisini Tukiwa form six, nadhan tulikua tumefunga shule tukiwa home, Dada yangu aliletewa mkanda Wa kikubwa na Rafiki yake baada ya Rafiki kuondoka tukawa tunauangalia sielewi ni nini kilitupata tukajikuta tumezini, mm kwangu ilikua ni Mara ya kwanza ila nadhan mwenzangu alikua tayari keshafanya huko nyuma Ikawa kila siku tunafanya wazazi wakiondoka. 

Kuja kustuka haoni siku zake akamwambia mama naye akamwambia baba Sijui niwaeleza lugha gani muweze kuelewa kilichotokea Ilikua ni mtiti akaambiwa aeleze ni nani aliempa mimba akawa anasingizia wanafunzi wenzie shuleni, wakifika shule anababaika anashindwa kutaja basi akafukuzwa shule hata mtihani Wa mwisho hakufanya Wakati hilo halijaisha biashara za Mzee zikaanza kuyumba vibaya vibaya na alikua na deni kubwa sana benki wakaja kuuza nyumba tunayokaa bado haikutosha Nyumba tuliyohamia ikapigwa mnada pia Mzee akapata stroke, tukaanza kuhangaika nae kila hospital, Mtihani Wa mwisho ulipofika sikuweza kufanya kitu nilikua naangalia tu makaratasi maana tulitoka maisha ya juu ghafla tukaporomoka hadi chini ndani ya miezi 9-12. 

Mzee akawa amefariki tukaenda kuzika kijijini Hakukua na chochote kilichobaki mjini si nyumba nini Tumezika kama Leo wiki moja mbele Dada akajifungua mapacha Wa kiume kama sisi tulivyo mapacha Baada ya ndugu kutawanyika na miezi minne kupita tukiwa bado kijijni maana tulipanga tuishi huko huko mjini hatukua na chochote mama aliniita akaniambia niende mjini nikaangalie matokeo yangu ndipo tunaweza kupanga tufanye nn Matokeo yalikua mabaya Usiku mmoja mama na babu wakaniita babu akaniambia chukua hawa ngombe ukauze wote utuachie watano tu Hii ndio mali pekee Mzee wako alioacha, walikua ngombe 200 Nikapewa baba zangu wadogo tukaenda mnadani tukauza nikapata pesa nyingi mno Nikaja dar kutafuta maisha na kiasi hicho cha pesa 

Nikawa nanunua ngombe mkoani naleta dar hadi mtaji ukaongezeka mara tatu Nikafungua biashara zingine na nikanunua kiwanja boko na nikajenga Nikarudi kijijini nikamchukua Dada yangu na watoto had I mkoani wakiwa na miaka mitano nikampangia nyumba na kumfungulia biashara lengo ni watoto waanze la kwanza hivyo walitakiwa maandalizi ya nursery Mama tulimwacha kijijini alikataa kabisa kuja mjini Siku moja tuliagiza pombe walau tusherehekee mafanikio maana hatukumini kama tungefika hapo Baada ya kunywa sana nikaona nikalale akanifuata chumbani na kuanza romance nikamzuia nikamwambia hatupaswi kurudia kosa hili, tushukuru huenda ni mpango Wa mungu Mzee kufariki kabla hajajua mm ndio nilikupa mimba Na bado hatujui siku mama akijua itakuaje Akaniambia yeye hataki mwanaume mwingine zadi yangu na kwamba ananipenda mm tu Nakuja kustuka hivi na boxer na vest ameshavitoa huku akiendelea na zoezi moyo wangu ulishakataa ila mwili ukawa dhaif tukawa tumezini.  

Tangu hapo huwa anakuja dar tunafanya nashindwa kuresist ile pressure Nikapata msichana mmoja dar alipokuja dar akatukuta nae kwangu alifanya fujo na kumpiga vibaya yule binti hadi majirani wakaniambia kumbe ulishaoa husemi, mi nashindwa kuwajibu Nikapata demu mwingine Dada yangu alipokuja akakagua simu akaona SMS za mapenzi akampigia akamtukana sana akamwambia yule demu eti nimeoa na nna watoto wawili demu akakimbia kimoja Nimepata Dada mmoja Wa benki tunapendana sana na tumepanga kuishi pamoja lakini kikwazo ni Dada yangu Akigundua tu ni balaa Sijui nimwambie huyu banker in advance kuhusu ili tatizo? Marafiki naombeni ushauri Maana mama mwenyewe anataka nioe nitulie  

Dada anasema nisijidanganye kuoa ni kazi bure Nikimwambia tafuta mtu wako na wewe uolewe hanielewi.  

Nifanye nini? Naogopa laana, naomba mnishauri

Wednesday, July 15

Emmanuel Mbasha Akutwa na Hatia ya Kesi ya Ubakaji



MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.
 
Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.
 
Mbele ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.
 
Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
 
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama ya siri ili kulinda haki ya binti huyo.
 
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Julai 23, mwaka huu ambapo Mbasha anatakiwa kufika na mawakili wake ili kujitetea dhidi ya shtaka hilo.

Friday, July 10

Vikao Vyote vya CCM Kufanyika Leo Na Majina ya 5 Bora na 3 Bora Yatajulikana leo


KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015.
 
Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.
 
Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau gan
richard blogs

Search This Blog