Monday, October 21

SHABIKI WA SIMBA DAR AFARIKI BAADA YA TIMU YAKE KUFUNGWA GOLI 3 BILA KIPINDI CHA KWANZA, KUSAFIRISHWA LEO NA ATAZIKWA KESHO MOROGORO NI SHABIKI MAARUFU SANA NCHINI, SOMA HAPA

 
Mwana dada ambae hakufahamika jina lake akiwa amezimia uwanjani baada kutokana na magoli ya Kiiza mawili ya mwisho ambapo dada huyo inadaiwa alikuwa mjamzito wa miezi 2 na baadae uliharibika kwa mshtuko huo. 
Mashabiki wa Simba wakiwa wamembeba mwenzao baada ya kuzimia kisa Kiiza kushinda goli la 3 huku timu yao ikiwa haina kitu kipindi cha kwanza. 
 Na Mwandishi Wetu
 Habari zilizotua mezani kwenye House of Media iliyopo maeneo ya Kawe kwenye Jengo la K-Net House floor ya 5 zinaema mzee mmoja maarufu nchini ambae ni shabiki wa timu ya Simba aliyefahamika kwa jina la  Ramadhani Mbande " Kindalindali" amefariki dunia jana maira ya saa kumi na moja na dakika 40 baada timu yake kufungwa magoli 3 bila kipindi cha kwanza.

Akiongea na Xdeejayz mmoja wa majirani wa mzee huyo mkazi wa Kigogo njiapanda ya Tabata Jijini Dar alisema mzee huyo alikuwa nyumbani akitizama mpira huyo pamoja na mwanae wa mwisho uliokuwa unarusha kupitia TBC1 kupitia Azam TV na baada ya mshambuliaji nyota Hamisi Kiiza Diego kuifungia timu yake magoli hayo mawili na kufanya kufikia idadi ya magoli matatu kwa mtungi hadi mapumnziko.  
Chanzo cha Xdeejayz kiliendelea kusema kuwa baada ya goli la tatu mzee ghafra alidondoka na kupoteza fahamu na baadae alikimbizwa Hospitali ya Amana na huko ndiko umauti ulikomfika. Hata hivyo mwili marehemu utasafirishwa leo kuelekea kijijini kwao Mang'ura Mkoani Morogoro.

Hata hivyo wakati wa tukio hilo likiendelea timu ya Simba jana ilifuta uteja kwa Yanga baada ya timu hizo kukutana msimu wa mwaka jana na Yanga kubamiza Simba goli 2 kwa bila na jana pia Simba waliponea chupuchupu baada ya kurudisha kwa shida magoli matatu aliyokuwa ameshafungwa na Yanga.
DADA SHABIKI WA SIMBA APOTEZA UJAUZITO UWANJANI KWA MAGOLI YA KIIZA!
Dada mmoja ambae hakufahamika nae alijikuta anapoteza uja uzito wake baada ya mshtuko wa timu yake kufungwa magoli ya harakaharaka na Yanga hadi timu hizo zinakwenda mapunziko Yanga ilikuwa imeikandamiza Simba goli 3 kwa mtungi.
Habari za uhakika zilizonaswa na papalazi wa Xdeejayz waliokuwa wamesambaa uwanja mzima ulishuhudia dada huyo akisitiliwa na watu wa mslaba mwekundu na taarifa zilizokuja baadae zilisema kuwa dada huyo alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na uliharibika hapo hapo kwa presure!

No comments:

Post a Comment

Search This Blog